
Wanasheria wanaomwakilisha Raila Odinga katika mahakama ya upeo,
wameeleza majaji saba sababu zao, za kutaka tangazo la mwenyekiti wa tume
huru ya uchaguzi,iebc Wafula Chebukati kuwa, Ruto ni mshindi wa uchaguzi wa urais, litupiliwe mbali.
Mwanasheria Julie Soweto, mmojawapo katika kundi linalomwakilisha mgombeawa urais, kwenye mrengo wa azimio la umoja Raila Odinga, ameambia mahakama
kuwa matokeo kwenye fomu kadhaa za thelathini na nne A, yanatofautiana.
Kulingana na B Soweto, kuna tofauti katika idadi ya matokeo, katika baadhi ya
fomu thelathini na nne A, zilizotumwa kwenye mtandao wa iebc, yale
yaliyofikishwa katika kituo cha kujumuisha kura ya kitaifa Bomas na yale
waliyopokezwa maejenti.
Vituo vilivyokaguliwa na upande wa raila ni kutoka kaunti za Kamega, Bomet na
Kiambu.
Soweto vilevile amesema kuwa, licha ya idadi hizo kutofautiana, fomu hizo
zilikuwa na vigezo na nambari za usalama zinazofanana, kura elfu nne, mia nne
sitini na tatu za Odinga zikiondolewa na kuongezewa William Ruto katika fomu
arobaini na moja zilizokaguliwa.
Ikizingatiwa pengo dogo kati ya ushindi wa William Ruto na kura za Raila Odinga
alivyotangaza Chebukati, soweto ameomba mahakama kutilia maanani swala hilo,
akisisitiza kuwa jumla ya kura anazodai zilitolewa katika kapu la Odinga zinatia
doa ushindi wa Ruto.
Na JACOB MACHESO