Huku mdahalo wa idadi ndogo ya wapiga kura kujitokeza kushiriki
uchaguzi mkuu wa Agosti 9 ukishamiri, maeneo manane yaliyoshiriki
uchaguzi pia yameshuhudia wapiga kura wachache, washikadau
mbalimbali wakidai ni kawaida kwa chaguzi ndogo kama hizi,
kushuhudia watu wachache wanaopiga kura.
Wyckliffe Oparanya anayehudumu Kakamega kwa mhula wa pili
amejiunga na wawaniaji wa Azimio la Umoja, Fernandez Barasa wa
Kakamega na Abdulswamad Nassir wa Mombasa kulalamikia idadi hiyo
ndogo ya wapiga kura.
Katika eneo bunge la Pokot Kusini, vijana wengi wamesusia zoezi hilo,
ikizingatiwa pia kuwa ni vijana wachache walijitokeza kujisajili kupiga
kura ikilinganishwa na wazee.


Cleophas Malala anayewania ugavana wa kakamega kupitia chama chaANC katika mrengo wa Kenya Kwanza kwa upande wake ameonyesha
kutoshangazwa na idadi ndogo ya wapiga kura, akisema atakayeshinda
kati ya wagombea ndilo swala kuu, bila kujali idadi ya wanaoshiriki
uchaguzi huo.
By JACOB MACHESO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here