Hali hii ya huzuni na kilio ndio iliyotawala katika familia ya mwendazake Dickson Inganga baada ya jamaa Yao kufariki akiwa kazini katika kiwanda Cha kusaga sukari Cha Mumias,baada ya kutumbukia kwenye bwela na kunywa sukari na kemikali kupita kiasi ambapo ilisababisha kifo chake.
wafanyakazi wa Kiwanda Cha Mumias wanalalmikia kuwa hawana vifaa vya kiusalama vya kufanyia kazi.
Mwendazake ndiye aliyekuwa tegemeo katika familia yake akiwa ameacha watoto Saba na mke moja.
Wafanyakazi hao sasa wanamtaka  mwanakandarasi kwa jina la Sarrai kufanya marekebisho katika kiwanda hicho kwani vifaa vingi vimeharibika na kuoza. 

Na Diana Eboso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here