Waajiri nchini, waraiwa kuwaruhusu wafanyakazi waliosajiliwa
katika kaunti mbili, maeneo bunge manne na wadi mbili
kushiriki haki yao ya kikatiba, tarehe ishirini na tisa agosti.
Maeneo hayo manane ambayo chaguzi zake zimeahirishwa
mara mbili ni kaunti za Kakamega na Mombasa, maeneo bunge
ya Kacheliba, Kitui Rural, Pokot Kusini na Rongai.
Maeneo mengine mawili yaliyoratibiwa kupiga kura siku hiyo ni
wadi ya Kwa Njenga kule Nairobi, na Nyaki Magharibi
inayopatikana Imenti Kaskazini.
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, ilisitisha chaguzi hizo
awali, kutokana na itilafu katika uchapishaji wa karatasi za
kupigia kura.
Na Jacob Macheso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here