
Ligi kuu ya mabingwa ulaya katika msimu huu wa 2022/2023 inatarajiwa kuanza mnamo tarehe sita mwezi wa tisa jumanne .
Mechi izi zilichezwa mwanzo miaka 68 zilizopita na kutengenezwa upya miaka 31 zilizoisha . Real madrid ambao kwa sasa ndio mabingwa watetezi katika kombe hilo ndio wameshinda mara kumi na tano ambayo ni recodi kubwa Zaidi ikilinganishwa na timu zingine katika mchuano huo .
Shirika la mipango lilitoa jedwali ambayo iko na jumla ya matimu 32 ambazo zimetawanywa kwa makundi 8 kila kundi likiwa na timu nne .

Kundi la kwanza kuna Ajax , Liverpool , Napoli na Rangers . katika kundi la pili kutakua na Porto , Athletico Madrid , Bayerleverkusen na Club brugge . Katika kundi la tatu kutakua na Bayern, Barcelona , intermilan na plzen . katika kundi la nne kutakua na Frankfurt , tottenham ,Sporting CP na Marseille. Katika kundi la tano , kutakua na AC Millan , Chelsea , Salzburg na Dinamo Zagreb . katika kundi la sita kutakua na real madrid , Leipzig , shakhktar doneski na celtic . katika kundi la saba kutakua na machester city , sevilla, borrusia Dortmund na Copenhagen . katika kundi la nane , kutakua na PSG, Juventus , Benfica na Haifa fc .
Msimu huu timu zote ambazo zimehushwa kwa mashindano haya zimejitahidi sana kwa hali na mali kwa kusajili wachezaji mabingwa ili kuhakikisha kuwa wanaleta mashindano makubwa sana.
Na Fantastone*