Siku ya jumatatu, kinara wa mrengo wa azimio Raila Odinga, alipeleka kesi kwenye mahakama kuu nchini, kupinga ushindi aliopewa mpinzani wake William Ruto, kama rais mteule. Odinga alipeleka kesi hiyo kwa kutoridhishwa na matokeo hayo, akisema kwamba kura hizo za urais hazikuhesabiwa kwa haki. Kesi hiyo sasa, inasikizwa na majaji saba wakiongozwa na jaji mkuu Martha Koome.

Kwenye kundi hilo la majaji saba, watatu kati yao wana uzoefu wa kuamua kesi kama hiyo, kwani walifanya uamuzi kama huo mwaka wa 2013, wakati wa kesi ya Odinga dhidi ya Uhuru Kenyatta, na wanne watakuwa wanafanya uamuzi huo kwa mara ya kwanza.

Jaji mkuu Martha Koome, ambaye ndiye anaongoza majaji hao, atakuwa anafanya uamuzi kwa mara ya kwanza. Yuko na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Nairobi, na chuo kikuu cha uingereza. Alikuwa mwanachama wa chama cha sheria cha kenya,. Mwaka wa 2011, alikuwa mmoja wa mahakama ya rufaa, na alikuwa mwenyekiti wa majaji nchini. Alichaguliwa kama jaji mkuu mwaka wa 2021 na rais Uhuru Kenyatta, na atakuwa anaongoza majaji wengine sita kuamua kesi hiyo ya odinga.

Martha Koome

Philomena Mbete Mwilu, ambaye ni naibu jaji mkuu, alikuwa mmoja wa majaji walioamua kesi ya odinga mwaka wa 2017. Yuko na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha nairobi, alikuwa wakili wa mahakama kuu mwaka wa 1984, aliwai kufanya kazi na kampuni ya majaji ya mutunga, amewahi kuwa mmoja wa mgao wa mazingira na ardhi katika mahakama kuu. Amekuwa jaji kwenye mahakama kuu mwaka wa 2012. Alitunukiwa tuzo ya dhahabu na rais Kenyatta mwaka wa 2017, mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kama naibu jaji mkuu mwaka wa 2016

Jaji William Ouko, amewahi kuwa rais wa mahakama ya rufaa tangu mwaka wa 2017, vilevile anashahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Nairobi, alianza kazi yake kama mwanasheria mwaka wa 1987 baada tu ya kumaliza masomo yake mwaka uo huo. Mwaka wa 1997, alichaguliwa kama mkuu wa Mahakama, na kupandishwa cheo mwaka wa 2002 na kuwa mwandishi mkuu wa mahakama. Ouko pia atakuwa anafanya uamuzi huo kwa mara ya kwanza

Jaji Njoki Ndungu, ambaye atakuwa anafanya uamuzi huo kwa mara ya pili, yuko na shahada ya sheria, na pia ana elimu ya haki kwa wanawake

Mohammed Ibrahim, pia ni jaji ambaye atakuwa anasikiza kesi hiyo. Alikuwa mmoja wa majaji mwaka wa 2017, lakini hakuweza kutoa uamuzi wake kutokana na hali yake ya kiafya. Amekuwa mmoja wa kampuni ya majaji ya waruiu

Jaji Smokin Wanjala, pia atakuwa anafanya uamuzi huo kwa mara ya pili, baada ya kushiriki kwenye kesi ya mwaka wa 2017. Yuko na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Nairobi, Columbia na Ubelgiji, na pia amekuwa mwalimu wa sheria chuo kikuu cha Nairobi kwa miaka 19.

Jaji wa mwisho ambaye pia atakuwa anafanya uamuzi wake kwa mara ya pili kwenye kesi kama hiyo ni jaji Isaac Lenaola, baada ya kushiriki kwenye kesi ya mwaka wa 2017.

Na David Amani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here