Ugumu wa maisha hupelekea wazazi kuchukua maamuzi yasiyo sahihi kwa watoto wao. Kisa cha hivi punde kutoka mjini nakuru zinahusu mwanamke mmoja wa miaka 23, ambaye anazuiliwa na maafisa wa polisi wa kuresoi kusini, kwa madai ya kumpa sumu mwanawe wa miaka minne, akitaka kumuuwa. Akithibitisha kisa hicho ocpd wa eneo hilo Lawari Jeremiah, amesema kwamba walipata habari hizo kutoka kwa ndugu ya mwanamke huyo na kumtia mbaroni

Kulingana Shadrack Kiprotich ambaye ni baba wa mhasiriwa, anasema kwamba mwanamke huyo ambaye walikuwa wametengana kwa muda, alimchukua mtoto huyo kwa madai ya kuenda naye kwa matanga na kumtambulisha

Aidha wazazi wamepewa wito wa kutowarusha ama kuwauwa watoto wao kwa ugumu wa maisha, kwani kuna vituo vingi vya kusaidia kuwalea watoto hao

By David Amani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here