Beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Italia na timu ya uingereza ya Chelsea Emerson Palmieri afanya maamuzi ya kujiunga na timu ya Westham kwa ada ya pauni milioni 13.

Kiungo huyo mwenye umri wa  miaka 28 alijiunga na Chelsea mwaka wa 2018 kutoka timu ya roma na akaweka sahihi ya kudumu Chelsea kwa miaka minne . alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Hull city katika nusu fainali za  kombe la FA na akatoa assist ambayo ilikua goli ya kwanza yake Olivier Giroud ambaye pia alikua ametoka arsenali.

Emerson ameweka mkataba baina yake na westham wa miaka mitano na itakamilika pindi pindi itakapofika mwaka wa 2027  . Chelsea wamemwachilia beki huyo kwa ada ya pauni milioni 13 na anamalizia medicals kisha atangazwe rasmi kama mchezaji wa westham .

Kwingineko ni kuwa mshambulizi matata wa timu ya arsenali Nicholas pepe ahusishwa na uhamisho kwa mkopo kuelekea timu ya nice . mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka taifa la ivory coast alijiunga na timu ya arsenali kutoka lille kwa ada ya pauni milioni 72 mwaka wa 2019 .amehusika kucheza mechi 80 na amefunga mabao 16 na kutoa assists 9 .

Nicholas pepe hajakua na msimu mzuri sana na anaonekana kudidimia sana katika mchezo wake . Nice fc wameonekana kuvutiwa sana na mchezaji huyu lakini arsenali hawako tayari kumwuza , arsenali wanaona bora kumpatiana kwa mkopo wa msimu mmoja . kwa sasa majadiliano baina ya timu hizi mbalI bado zinaendelea na iwapo watafkia kuelewana atatangazwa rasmi kama mchezaji wa nice .

Arsenali wanamipango ya iwapo watamuachilia nicholas pepe watafanya usajili wa mshambulizi kutoka ureno anayeichezea timu ya wolves .Pia wanaweza msajili Mousa Diaby ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Leverkusen . kumsajili diaby kuna ugumu kwa arsenali kwa sababu bado mwenyewe hajaamua kufanya uhamisho hadi yuko katika harakati ya kuweka mkataba mwingine na Leverkusen . hadi sasa hakuna majadiliano baina ya Leverkusen na arsenali na iwapo kutakua na mazungumzo Mousa Diabi atatangazwa kama mshambuliaji mpya wa arsenali

*By Fantastone*

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here