Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ujerumani Ilkay Gundogan achaguliwa rasmi kuwa nahodha wa timu ya uingereza ya Manchester City.

Gundogan amekua kiungo muhimu sana katika timu ya Manchester city kwa kufunga mabao muhimu zaidi . kwa mara kadhaa amekua mfungaji wa mabao mengi katika timu na msimu uliopia alifunga mabao muhimu ambayo iliwezesha Manchester city kuibuka washindi katika ligi kuu ya uingereza . tangu kutoka kwake Borussia Dortmund , amekua mchezaji ambaye anajituma Zaidi katika mechi zake zote .

Gundogan amemridhi mchezaji aliyekua wa taifa la brazil fernandinho luiz rosa ambaye pia alikua kiungo wa kati na alishinda ligi kuu ya uingereza mara tano baada ya kuichezea machester city kwa miaka tisa . fernandinho alijiunga na timu ya club athletico paranaence ilioko nchini brazil .akiwa nahodha wa Manchester city alishinda ligi kuu mara mbili  na capital one mara moja . kwa ujumla , kiungo huyo mwenye umri wa miaka 37 alishinda mataji 12 katika timu ya Manchester city , alishinda capital one mara 6 , premier league mara 5 , FA cup mara moja , super cup mara 2 baada ya kucheza mechi 264.

Kelvin de bruine ndiye ambaye atakua naibu wa ilaky gundogan katika msimu huu wa 2022-2023 . coacher wa Manchester city joseph pep Guardiola anaamini kwamba viungo hawa wawili watamsaidia sana kushinda mataji katika msimu huu . pia katika uongozi wake pale etihard alimwongeza rodri kama kiongozi pia . anaamini sana hawa wachezaji na michezo wanayoicheza pale etihard . ujuzi kutoka Belgium yake kelvin debruin , ujuzi kutoka uhispania wake rodri na pia ya ujerumani yake gundogan .   

Kwingineko ni kuwa kuna tetesi katika mitandao ya kijamii ikiwemo twita kuwa binadamu tajiri sana ulimwenguni Elon Mursk ana madai ya kununua timu ya uingereza ya Manchester united kutoka kwa the glazers family iliyoko marekani . III ni baada ya timu iyo kuwa na  matokea mabaya . katika msimu huu wa 2022-2023 manchester united wamecheza mechi mbili na hakuna yeyote ambayo wameshinda , mechi ya kwanza ilikua dhidi ya brighton ambayo iliisha 2-1 ., mechi ya pili ambayo ilichezwa wikendi Manchester united walipigwa 4-0 . mashabiki wana Imani kuwa wakibadilisha uridhi huo utabadilisha matokeo ya timu nzima

FANTASTONE   

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here