Wingu la siasa na uchaguzi limekua na madhara mengi sana katika sekta mbalimbali za  kitaifa na mojawapo ambayo imeadhirika sana ni sekta ya michezo .

Ni huu mwaka mnamo tarehe 25 februari ambapo timu utaifa ya kenya ya harambee stars walipigwa marufuku ya michezo ya afcon na vyama vya michezo ikiwemo fkf na fifa , baadae waziri wa michezo amina mohammed akatangaza wazi kuwa kenya haitahusika kwenye mashindano hayo ya afcon .

Harambee stars walishiriki michezo hiyo mwisho mwaka wa 2019 na walikua kwenye kundi moja na Senegal , algeria na Tanzania , kenya walishinda mechi moja tu dhidi ya Tanzania ambayo iliisha 3-2.

Msimu huu kenya walikua kwenye kundi ambalo kulikua na Cameroon , Namibia na Burundi . kenya ilitolewa na kuwacha makundi mengine yakiendelea.

Wengi walipongeza uamuzi wake Amina Mohammed wakisema kwamba itaweka mambo wazi na hakutakua na ufisadi tena .

Serikali na wanasiasa wa taifa la Kenya wamechangia sana pakubwa katika kudhoofisha michezo za kenya . wao wenyewe hawajazingatia swala la ugawaji imara wa ujasiriamali kwenye sekta zote ,kama soka haijazingatiwa sana . wanatenga pesa nyingi sana za kufanya kampeni kushinda wanazozitenga kwa minajili ya michezo

Hata katika bodi ya uchaguzi wa viongozi katika timu ya utaifa kumejawa na mapendeleo chungu nzima . wakati mwingine wanasiasa wenyewe wanahusika katika kuchagua viongozi hawa ambao hawajui majukumu yao .

Nchi kama senegali viongozi wa soka ni watu ambao wanajua vizuri soka na wamehusika kucheza kwenye umri wao mdogo.alieu cisse coacher wa Senegal alichezea timu hiyo ya utaifa mwaka wa 2002 kwenye mashindano ya afcon .

Hata hivyo kwenye riadha , wakenya walituwakilisha vizuri sana mjini Birmingham Oregon Ferdinand omanyala aliongoza kundi nzima kwa kushinda dhahabu kwa mbio za mita 100 za wanaume .beatrice chebet , hellen obiri , Margaret chelimo , conseslas kipruto na wengine kadhaa walishinda medali tofauti tofauti .

Wanamichezo wanaiomba serikali ambayo itachaguliwa na wananchi kuwa waipe pia michezo kipaombele na wakigawa raslimali wawe pia wakwanza kukumbukwa .

Fantastone Mutama

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here