Serikali, kupitia wizara ya Teknolojia na habari mara nyingine imewahakikishia Wakenya kuwa huduma
za mitandao, ikiwemo Meta, Twitter na Whatsapp haitakatizwa katika kipindi hiki cha uchakuzi.
Akizungumza katika mkutano na maafisa wakuu wa kampuni za mawasiliano, waziri wa teknolojia na
habari, Joe Mucheru ameongeza kuwa wizara yake haina mipango yoyote ya kuathiri matokeo ya
uchakuzi kupitia udukuzi, wanavyodai baadhi ya wanasiasa.
Siku chache zilizopita, tume ya Uwiano na utangamano nchini (NCIC,) ilikumbana na ubishi mkali kutoka
kwa viongozi wa kisiasa kwa pendekezo lake la kuzima mitandao katika kipindi cha uchaguzi mkuu, ili
kukabili semi za chuki na uchochezi.

Usemi wa Mucheru umeoana na ule wa waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I, ambaye pia kwa
upande wake awali alipuzilia mbali tetesi za serikali kuhitilafu huduma za mitandao ya kijamii.
Jacob Macheso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here