Beki wa kushoto wa timu ya utaifa ya Brazil na timu ya uingereza ya Manchester United Alex Telles ahusishwa na uhamisho wa timu ya Sevilla Uhispania.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 anahisi kwamba huenda asipate muda mzuri wa kucheza pale old Trafford , hii ni kwa sababu ya usajili wake Tyrell Malacia katika nafasi hiyo hiyo . Hata hivyo sevilla wameonyesha nia na maksudi ya kumsajili beki huyo.

Pia mlinzi wa Ivory Coast na timu ya Manchester United Erick Baily mwenye umri wa miaka 28 anahisi kuwa akiendelea kutumikia Manchester United huenda atakosa kupata nafasi nzuri ya kucheza pale old Trafford . Mlinzi huyo alianza kupata shauku pindi tu Lisandro Martinez alivyotoka Ajax na kuingia old Trafford . Bailey huenda akajiunga na timu ya uhispania ya Sevilla .

Kwingineko ni kuwa Kocha wa Manchester city Joseph Pep Guardiola amemmezea mate beki wa kushoto wa utaifa ya uhispania na timu ya Benfica Alejandro Grimaldo . Grimaldo alikua na msimu mzuri msimu uliopita kwa kucheza mechi 29 na kufunga mabao 5 na kutoa assists 5 .

Joao Cancello ndiye aliyekuwa mchezaji wa kipekee katika katika timu nzima ya Manchester city kucheza mechi mingi Zaidi ya wachezaji wengine wote kwenye timu . alicheza mechi 36 akafunga bao moja na kutoa assists za mabao 7 . Pep Guardiola anaona kwamba akimsajili Grimaldo atakuwa wa msaada sana kwa cancello katika kujiimarisha na kupata muda mzuri sana wa mapumziko .

Benfica wanataka ada ya pauni millioni 20 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. Hadi sasa Manchester city hawajawasilisha chochote . hata hivyo arsenali pia wamewasilisha mazungumzo yao katika kumsajili Grimaldo , wamewasilisha ada ya pauni millioni 34.

Tangu kuondoka kwake Alexandre zinchenko Guardiola hakuwa amepata beki mwingine katika nafasi hiyo .anatumai kuwa Grimaldo ndiye mchezaji anayefaa Zaidi katika nafasi hiyo.

FANTASTONE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here