Jamii ya waluhya, haswa wabukusu kutoka magharibi mwa kenya, wameanza kushiriki sherehe za
kitamaduni, za upashaji tohara wa mwaka huu. Kidesturi sherehe hizi huandaliwa mwezi wa agosti,
wakaazi katika kijiji cha Munyikina katika eneo bunge la Webuye Magharibi katika jimbo la bungoma,
wakikataa kubaki nyuma katika shughuli za kuidhinisha usemi wa wahenga kuwa, “Mwacha mila ni
mtumwa.”
Katika boma la mzee Matthews Waswa Walekhwa ambaye ni kipofu, kijanake mwenye umri wa miaka
kumi na saba alipaswa kupashwa tohara katika msimu uliopita mwaka wa elfu mbili na ishirini, ila janga
la korona likawa kizuizi.
Tofauti na kawaida ya sherehe hizi ambapo ng’ombe huchinjwa na wakaazi kubugia pombe, msimu huu
hali ni tofauti, kwani mzee huyu amelazimika kuchinja bata pekee.
Katika boma la mzee Wyckliffe Nyongesa, siku kuu iling’oa nanga majira ya saa kumi na moja asubuhi,
wakati kijana anayepaswa kupashwa tohara alipelekwa mtoni na kurejeshwa mwendo wa saa mbili
kabla ya kupitia kisu cha ngariba.
Babake kijana huyo, mzee Wyckliffe Nyongesa na ngariba Nabwera Wanasyoka, wakitaka jamii ya
Wabukusu kuendeleza mila hiyo, wakisema vijana wanaopitia itikadi hiyo huwa na heshima na maadii
mema katika jamii.
Milton Wafula ni ngariba na amewapasha tohara vijana kumi na watano.
Mwaka huu, jamii hiyo inafunga rika la Bakikwameti ili kuanza rika la Bakananachi katika msimu ujao
mwaka wa 2024
JACOB MACHESO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here