Midfielder wa timu ya utaifa ya Argentina na timu ya ufaranza ya PSG  Lionnel Messi amemezewa mate na timu ya uhispania alioichezea awali ya Barcelona na timu ya marekani ya MLS .

Kandarasi ya nyota huyo mwenye umri wa 35 unafikia ukingoni mnamo mwaka ujao . PSG wanamipango ya kumuongezea kandarasi nyingine kwa sababu ya uhusiano wake mzuri na timu nzima , pia wanaamini kuwa atawasaidia kutimiza ndoto yao ya siku zote ya kushinda champiosleague .

Laporta ambaye ndiye rais wa Barcelona ameonekana kwenye mihadhara mingi akizungumzia kuhusu usajili wake messi kwenye kilabu ya Barcelona . kocha wa Barcelona Xavi Hernandez anaamini kuwa usajili wa messi utaleta ukamilifu katika timu nzima ya Barcelona pia italeta ushindano mkubwa kwenye mashindano yote na itamuwezesha kushinda mataji mengi . hadi sasa , Barcelona bado hawajafanya mazungumzo na messi , wanamipango tu ya kuanza kumpigia simu wakati ukifika .

Ndoto na azma ya lionel messi siku zote  ilikua ni kumalizia uchezaji wake MLS  kule marekani . Kwa sasa hajafanya mazunguzo yoyote na timu yoyote na hajahusishwa na timu yeyote kwenye mazungumzo yoyote . anaendelea na matayarisho yake ya kucheza kwenye kombe kuu la dunia ya world cup 2022 itakayoanza December.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here