Rais Uhuru Kenyatta akiwa katika siku za lala salama kabla ya
Kumpisha mrithi wake katika ikulu, mihula yake miwili imekuwa na
Panda-shuka katika uongozi wa taifa, siku chache zilizopita
akiwaongoza wafanyakazi wa ikulu katika hafla ya kustaafu kwake.
Wakenya wamekuwa na hisia mseto kuhusiana na uongozi wa rais
Kenyatta.
Zachariah Barasa aliye mwaniaji wa ubunge Sirisia katika jimbo la
Bungoma, kwa maoni yake asema, serikali ya Jubilee ina mengi ya
Kujivunia, japo eneo la magharibi linaonekana kusahaulika katika
Miradi ya maendeleo liilinganishwa na maeneo mengine.

Rais Kenyatta mara si moja, amesifia salamu zake za heri za machi
Mwalka wa elfu mbili kumi na nane, na aliyekuwa waziri mkuu Raila
Odinga, akisema uhusiano wake mwema na Odinga ndio chanzo cha
Maendeleo na amani katika mhula huu wa pili, akitofautiana na naibu
Wake William Ruto anayeshikilia kuwa ukaribu wa raila serikalini
Ulibadili nia ya serikali, akiongeza kuwa mchakato wa kubadilisha
Katiba bbi ulichukua nafasi ya agenda nne kuu za jubilee.
Geofrey nyage na Patrick Okumu, ambao ni wakaazi wa Nairobi,
Wanakubaliana kuwa Jubilee imefeli wakenya katika vita dhidi ya
Ufisadi.
Viongozi waraiwa kutimiza agenda zao kwa manufaa ya jamii, Ann
Kerubo aliye mkaazi wa Kisii, akiwakumbusha wawaniaji wa vyeo
Mbalimbali kuwa ahadi ni deni, dawa yake ikiwa ni kulipa.
Jacob Macheso