
Waziri wa elimu profesa George Magoha amesema kuwa shule zote humu nchini zinapaswa kufungwa hapo kesho.
Hii ni kinyume na kauli yake ya hapo awali ambapo waziri huyo alikuwa amesema kuwa shule zote zitafungwa tarehe sita mwezi wa nane na kufunguliwa tarehe kumi na Tano.
Kwa sasa shule zitafungwa hapo kesho na kufunguliwa tarehe kumi na moja. Mabadiliko haya yamefanyika ili kuhakikisha kuwa kuna maandalizi mwafaka ya uchaguzi mkuu ujao. Waziri Magoha amedokeza pia , iwapo kutakuwa na marudio ya uchaguzi, washikadau katika sekta ya elimu watahitajika kujadili jinsi ya kupambana na swala la wanafunzi kupotezewa muda .