
Uchaguzi mkuu unapokaribia nchini, amani yahubiriwa katika pembe
Zote za taifa. Serikali imewahakikishia wakenya usalama hasa wakati
Na baada ya uchaguzi. Macho yote ya serikali, hata hivyo,
Yanaonekana kukodolea tu, agosti tisa, huku baadhi ya wakenya
Wakikumbwa na utovu wa usalama.
John wafula, aliye mmiliki na mwekezaji katika shamba linaloitwa the
Black swan, katika kijiji cha bondeni, lokesheni ya machewa, katika
Eneo bunge la saboti kaunti ya trans nzoia, anakadiria hasara ya
Takriban shilingi milioni mbili, katika shamba lake la ekari arobaini na
Mbili.
Ijumaa ya tarehe ishirini na mbili julai, genge la wahalifu lilivamia
Shamba hilo usiku, likkangamiza na kuiba mali, ikiwemo mizinga mipya
Ya nyuki thelathini na mitano, tanki za maji, nyua, nyumba na mavazi
Wanayotumia wahudumu wa shamba hilo, na vilevile kuchinja na
Kuiba mifugo.
Joseph simiyu, aliye meneja katika shamba hilo, asema maisha yake na
Ya mwajiri wake john yamo hatarini, akiongeza kuwa, wavamizi hao
Walinuia kuyakatisha maisha yake, swala lililombidi kukesha kwenye
Baridi msituni kuyaokoa maisha yake.
Runinga ya tandao ilizuru bondeni katika lokesheni ya machewa,
Mahala pa mkasa, japo kwa ugumu ukizingatiwa uduni wa miundo
Msingi, ikiwemo barabara, ugumu wa kufikia eneo hili ukihitilafu
Pakubwa, upesi wa vitengo vya usalama kuwanusuru wananchi
Patokeapo mikasa kama hii, wakaazi kwa kero, wakikiri kusahaulika na
Viongozi waliowachagua, na kuongeza kuwa serikali imefeli eneo hili
Katika ukuaji wa maendeleo.
Zaidi ya juma sasa tangu uvamizi huo kufanyika, mwekezaji john
Wafula akaaye marekani, na meneja joseph simiyu anayehudumu
Katika shamba hilo, bado wasubiri sheria kuchukua mkondo wake
Dhidi ya wavamizi hao, usemi maarufu kuwa serikali ina mkono
Mrefu, kwao ikisalia tu ndoto ya mchana, wakiendelea kulilia haki,
Kwani haki inayocheleweshwa ni sawa na haki inayonyimwa.
Jamii hii kwenye shamba la the black swan, imebaki na kitendawili cha,
‘je, tutalia hadi lini?’ mwenye kukitegua kitendawili hiki akiwa waziri
Wa usalama wa ndani, dakta fred matiang’i kwa ushirikiano na ocs
Katika kaunti ya trans-nzoia, matumaini ya kufanyiwa haki kutumia
Vitengo vya usalama vya eneo hili yakididimia kila kuchao, kwa kuwa
Hadi sasa hakuna mshukiwa aliyetiwa mbaroni licha ya maafisa wa
Polisi kuaminika kuwafahamu wahusika, kwani wavamizi hao
Waliwatayarisha polisi hao na kuwapa vitisho katika mazungumzo ya
Moja kwa moja kabla ya uvamizi, na polisi hao vilevile wakawarai
Wavamizi kurejesha mbuzi mmoja, kulingana na meneja joseph
Anayeshikilia kuwa matunda ya uchunguzi wa mwendo wa kobe
Unaofanywa na polisi hao huenda usizae matunda.
Jacob Macheso