
Timu ya ujerumani Borussia Dortmund yammezea mate mshambulizi wa timu ya utaifa ya Uruguay na timu ya uingereza ya manchester united Edison Cavani.
Kandarasi ya mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 35 imefika ukingoni pale old Trafford na kwa sasa ni free agent .
Cavani anajulikana sana na ujuzi wake wa kipekee wa kufunga mabao na anajulikana sana kwa jina lake la lakabu kama bullfighter . Amecheza katika ligi tofauti tofauti , na akiwa PSG alivunja rekodi kwa kuwa mchezaji mwenye mabao mengi sana katika ligi ya ufaranza kabla ya kuachiliwa kama free agent na kujiunga na timu ya uingereza ya Manchester united .

Kabla ya michezo ya kombe la dunia world cup qualification ya mwaka wa 2018 ,alifungia timu yake ya utaifa Uruguay mabao 10 akaibuka kama top scorer na kuiwezesha timu yake kufuzu kuingia katika mashindano ya kidunia ya kandanda , world cup.iwapo kutakua na maelewano baina ya Manchester united na borrusia Dortmund cavani atatangazwa kama mchezaji wa Dortmund kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa .
Kwingineko ni kuwa mshambuliaji matata wa timu ya athletico madrid Diego Costa anamezewa mate na timu ya Roy Vallecano ya south America . kandarasi ya mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 33 imefika kikomo pale Athletico Madrid na kwa sasa ni free agent .iwapo kutakua na maelewano baina ya izi timu Diego Costa atatangazwa kama mchezaji wa Roy vallecano .
Vile vile , wakurugenzi na kocha wa timu ya Manchester united wametangaza kuwa Christiano Ronaldo hauzwi tena na anatarajiwa kuwa katika zoezi na wachezaji wenzake . Mendes ajaridhishwa na msimamo ule na amesema atafanya mkutano wa majadiliano baina yake na Erick Ten Hag ili kutoa suluhu FANTASTONE MUTAMA