uchaguzi huru na haki, amani na utangamano

0
8

Wiki mbili kabla ya agosti tisa, wakenya wakisubiri kwa hamu kushiriki uchaguzi mkuu, washika dau mbalimbali wameendelea kuweka mikakati kabambe ya uchaguzi huru na haki, amani na utangamano ukipewa kipao mbele, na makundi na mashirika kadhaa ya kijamii. Kaunti ya uasin gishu ikitajwa awali na tume ya kitaifa ya uwiano na utangamano NCIC, kuwa moja kati ya sita zilizo katika hatari ya kushuhudia vurugu zinazohusiana na uchaguzi, leo hi wafanyibiashara ,viongozi wa kidini na wadau wengine wamekutana kujadili maswala ya amani kuhusiana na uchaguzi ujao.

Akiahidi kuwahusisha wagombeaji wa viti mbalimbali,  kamishna wa kaunti ya uasin gishu pia amekiri kuwa kaunti hiyo ni salama na amani itadumishwa, usemi uliopigwa jeki na erick, aliye naibu mwenyekiti wa kongamano la wafanyibiashara nchini, kinyume na utabiri wa awali wa tume ya uwiano na utangamano nchini ncic.

Kamishna wa uasin gishu vilevile ametetea uamuzi wa kutoruhusu uuzaji wa vileo wakati wa uchaguzi katika kaunti hiyo, akisema wawakilishi wa wafanyibiashara na washikadau wengine walihusishwa katika maamuzi hayo, yanayonuia kuhakikisha kuwa amani inadumishwa na wananchi wanajitiokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu.

by Jacob macheso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here